November 22, 2013





Kipa wa Gor Mahia ya Kenya, Ivo Mapunda amesema kitendo cha Simba kumpa ajira Kocha Zdravko Logarusic ni jambo muhimu kwa kuwa kocha huyo ana uwezo mkubwa wa kufundisha.


Ivo ambaye sasa yupo nchini kwenye kambi ya kikosi cha Kilimanjaro Stars, kinachojiandaa na Kombe la Chalenji, aliwahi kufundishwa na Logarusic katika timu ya Gor Mahia.

Amesema Logarusic, raia wa Croatia, anaweza kuisaidia Simba kwa kuwa aliwahi kuisaidia Gor Mahia kutoka nafasi ya kumi katika msimamo wa Ligi Kuu Kenya na kuipeleka mpaka nafasi ya pili, ambapo ilisalia kidogo timu hiyo iwe bingwa.

“Niseme ule ukweli kwamba Simba imepata kocha bora kwa hadhi yao, kwa kipindi cha miezi sita niliyokaa naye pale Gor (Mahia), kilitosha kuuelewa ubora wake kwa kazi aliyoifanya pale,” alisema Ivo na kuongeza:

“Kwanza sifa moja kubwa aliyonayo Logarusic ni kupenda kuona timu yake inashinda, hapendi kupoteza mechi, sasa hapo ndipo wachezaji wa Simba wanatakiwa kujiandaa na hilo, lakini ukweli ni kwamba ni kocha mzuri na yupo makini sana.”

Wakati huohuo, imefahamika kuwa kocha huyo mpya ameomba mkataba wa miezi sita kwa lengo la kumalizia duru la raundi ya pili.

Aidha, Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen amesema Mapunda ameonyesha uwezo wa juu licha ya kuwa amemuita kikosini hapo kwa mara ya kwanza tangu alipoanza kuinoa timu hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic