November 16, 2013

KISAKA (KULIA) AKIWA NA KOCHA WA ZAMANI WA SIMBA, PATRICK LIEWIG NA MENEJA, MOSES BASENA

Kocha wa makipa wa Simba, James Kisaka bado anakumbukwa kutokana na uwezo wake mkubwa aliokuwa nao wakati akiwa kipa.


Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF), Jacob ‘Ghost’ Mulee amesema aliwahi kucheza kikosi kimoja na Kisaka na alikuwa na uwezo mkubwa sana.

“Namkumbuka sana Kisaka, alikuwa na uwezo wa juu akiwa langoni wakati tukicheza pamoja katika timu ya Volcano,” alisema.
“Unajua mimi nilikuwa kipa ninayechipukia na Kisaka hakuwa mchoyo kwa mafunzo, namkumbuka sana.”


Mulee pia amewahi kuwa kocha wa Kenya, Harambee Stars na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuchukua Kombe la Chalenji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic