November 16, 2013


Mkurugenzi wa Ufundi wa Coastal Union, Nassor Bin Slum amesema kipa Shabani Kado anaendelea kubaki katika kikosi hicho.



Bin Slum alikuwa anazungumzia kuhusiana na Simba, jana kulizagaa taarifa kwamba kipa huyo yuko mbioni kujiunga na Simba.

Lakini Bin Slum alisisitiza kwamba kipa huyo ana mkataba na ataendelea kuichezwa Coastal

"Kado ana mkataba hapa, Simba hawawezi kuzungumza naye kabla ya kufika kwetu, hivyo Kado bado yuko Coastal," alisema.

Simba imekuwa ikihaha kusaka kipa ikiwa ni siku chache baada ya kumuacha kipa Juma Kaseja aliyekuwa nahodha wa timu hiyo kwa madai ya kuteremka kiwango.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic