November 6, 2013




Kocha wa zamani wa Simba, Patrick Liewig amesema uvumilivu umekwisha kwake.


Amesema amekuwa akipewa ahadi kila siku na Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage.

Liewig amesema Rage kila mara amekuwa akimuahidi kukutana naye bila ya mafanikio kwa madai yuko busy.

“Kweli najua yuko busy, lakini vizuri atekeleze ahadi zake anazonipa, sipendi kulumbana na watu wa Simba.

“Nimekuwa muungwana na mvumilivu lakini sasa nimechoka kuhusiana na suala hili na hasa mwenyekiti, kweli ananiumiza sana na ajue nimetoka mbali kuja hapa kwa ajili ya 
walichoniahidi,” alisema Liewig raia wa Ufaransa.

Jana alisema, Simba waliahidi kumlipa dola 10,000 kati ya 16,000 anazowadai lakini hawakutekeleza ahadi.

Badala yake wakamlipa dola 7,000 kabla ya kuongeza dola 1000 na kuwa 8000.
“Sasa nawadai dola 8,850 ambazo wanatakiwa wanilipe fedha zangu zilizobaki, tayari nimeanza kuwa na hofu,” alisema Liewig.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic