November 6, 2013


Real Madrid imetoa sare ya mabao 2-2 ikiwa ugenini dhidi ya Juventus na Cristiano Ronaldo na Bale, kila mmoja akifunga bao moja.

Katika mechi  hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Juventus walipata mabao yao mawili kupitia Vidal kwa mkwaju wa penalti na Llolente kwa kichwa.




Manchester City wao wakafanya kweli kwa kushinda mabao 5-2 dhidi ya CSKA Moscow huku Kun Aguero akipiga mbili na Nagredo akipiga hat trick.

Mechi nyingine FC Kopenhagen ikaichapa Galatasaray bao 1-0, Shaktar ikatoka sare ya bila kufungana na Beyer Leverkusen sawa na Manchester United ikabanwa na Real Sociedad ikiwa ugenini.




Mabingwa Bayern Munich wao kwa tabu wakiwa ugenini wameshinda kwa bao 1-0 dhidi ya Viktoria Plzen mfungaji akiwa ni Mandzukic.

Zlatan Ibrahimovic naye akaendelea kuonyesha ubora wake baada ya kuisaidia PSG kupata sare ya bao 1-1 baada ya kufunga bao lakini wageni Anderlecht ya Ubeligiji wakawa wabishi na kusawazisha.
.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic