November 17, 2013

AMROUCHE



Mechi ya kirafiki kati ya Taifa Stars dhidi ya Harambee Stars iliyopangwa kuchezwa kesho imeyeyuka.

Kocha Mkuu wa Kenya, Adel Amrouche amethibitisha kuwa mechi hiyo kesho haitakuwepo.

“Kweli hakutakuwa na mechi na matatizo yametokea hapa Kenya, wachezaji hawakupatikana kwa wakati unaotakiwa.

“Waambie mashabiki wa Tanzania nimesikitika kutokuja kucheza,” alisema.

“Nawaheshimu na mashabiki wa soka wa Tanzania ambao wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao. Huenda siku nyingine tutakuja na kucheza hapo.”

Mechi hiyo ilipangwa kuchezwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic