Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Millen Happiness
Magese amewataka watu binafsi na makampuni mbalimbali kujitokeza kwa wingi
katika kusaidia tasnia ya elimu hasa katika maeneo yasiyopewa kipaumbele ili
kuwaokoa watoto wa maeneo hayo kutotumbukia katika vitendo visivyo vya
kimaadili.
Rai hiyo ameitoa wakati alipotembelea miradi yake aliyoifadhili ya
ujenzi wa vyumba vya madarasa na utengenezaji wa madawati.
Ujenzi wa madarsa unaendelea katika shule ya msingi
Mjimwema iliyopo manispaa ya Mtwara ambapo mradi wa kutengeneza madawati
ulikabidhiwa kwa vikundi mbalimbali vya wajasiriamali mkoani hapo kwa mpango
maalum kupitia ofisi ya mkuu wa Wilaya, Mheshimiwa Wilman Ndile.
Jumla ya
madawati hamsini na tano (55) yenye thamani ya shilingi milioni tano yalikuwa
tayari yameshatengenezwa kama walivyoahidi wajasiria mali hao wakati
wakikabidhiwa kazi ya utengenezaji wa madawati hayo.
Madawati hayo yalikabidhiwa rasmi na Millen yalikabidhiwa
kwa wanafunzi wa shule ya msingi Lilungu.
Kwa upande wa afisa elimu wa manispaa ya Mtwara Frola
Aloys amewataka wadau wa elimu kuonesha uzalendo wa hali ya juu kwa maeneo ya
Kusini mwa Tanzania huku mkuu wa shule ya msingi Lilungu Abdul Nangomwa
akielezea changamoto zinazoendelea kuikumba sekta ya elimu katika shule za
msingi wilayani Mtwara.
Mbali na kukabidhi madawati Millen aligtembelea ujenzi
unaoendelea shule ya msingi Mjimwema na kutoa zawadi ya madaftari napenseli kwa
wanafunzi hao ambapo mpaka sasa shule in mikondo mitatu ambayo ni kuanzia
darasa la awali mpaka darasa la pili.
Ziara hiyo ya mrembo huyo aliyewahi kushika taji la Miss
Tanzania mwaka 2001, ni mwendelezo wa shughuli za kijamii anazozifanya nchini
Tanzania hasa katika kusaidia makundi yenye mahitaji maalumu na yale yasiyopewa
kipaumbele.
Mwanzoni mwa mwaka huu Millen Magese alitoa kiasi cha
shilingi milioni kumi na tano katika kusaidia huduma hiyo ya elimu katika
manispaa ya Mtwara.
0 COMMENTS:
Post a Comment