Mechi
ya kwanza ya raundi ya michuano ya Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika kwa wanawake
chini ya miaka 20 kati ya Tanzania (Tanzanite) na Afrika Kusini iliyokuwa
ichezwe Mwanza sasa itafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Baada ya ukaguzi uliofanywa na
maofisa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imebainika uwanja huo
unatakiwa ufanyiwe marekebisho ambayo hayawezi kuwahi Desemba 7 mwaka huu, siku
ambayo ndiyo mechi hiyo inatakiwa kuchezwa.
Vyumba vya wachezaji vya
uwanja huo ndilo eneo ambalo linatakiwa kufanyiwa marekebisho makubwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment