November 11, 2013

 
NYAMWEYA (KUSHOTO) AKIWA NA KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA KENYA, HARAMBEE STARS, ADEL AMROUCHE. HAPA ALIKUWA AKIONYEESHA TUZO ALIYOWAHI KUPEWA NA RAIS MSTAAFU WA KENYA SASA, MWAI KIBAKI.


Na Saleh Ally, Nairobi
Gumzo kubwa la kisiasa katika nchi za Afrika Mashariki katika kipindi hiki ni kuhusiana na mvutano mkubwa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao unazidi kupata kasi.


Uamuzi wa Uganda, Rwanda na Kenya kuwa zinakutaka bila kuihusisha Tanzania na Burundi zimekuwa zikielezwa kama sehemu ya kuzitenga nchi hizo, huku kukiwa na taarifa kwamba Rwanda ndiyo chanzo katika hilo kwa kuwa Tanzania imeamua kupeleka majeshi nchini DR Congo na kuwasambaratisha wapinzani wa M23 ambao baadhi ya nchi zina maslahi nao.
AKIWA OFISINI KWAKE

Kila nchi imekuwa ikikanusha kuhusiana na M23, lakini hakuna cha kuficha kwamba mambo sasa si mazuri na kumekuwa na mvutano ambao ni ufa kwenye jumuiya hiyo.
Rais wa Shirikisho la Soka la Kenya (KFF), Sam Nyamweya ndiye kiongozi mkongwe zaidi wa juu wa soka anayeongoza kwa kipindi hiki.

Tanzania ina kiongozi wa juu mpya, Jamal Malinzi hali kadhalika Uganda. Nyamweya anabaki kuwa mkongwe wa viongozi wote wa juu na mwenye anajiita baba.

Katika mahojiano maalum na gazeti hili ofisini kwake jijini Nairobi, Nyamweya anasema huu ndiyo wakati mwafaka wa soka kuonyesha nguvu yake na ikiwezekana kurudisha udugu na kuongeza ushirikiano unaoyumba wa Afrika Mashariki na Kati.
AKIWA NA SALEH ALLY ALIPOMTEMBELEA NYUMBANI KWAKE JIJINI NAIROBI

“Soka linaweza, huu mchezo una nguvu sana na katika nchi nyingi sana umetumika kufanya kazi ngumu kama hizo ambazo zilikuwa zimeshindikana kwa kila namba,” anasema Nyamweya.
Afrika Mashariki:

Watu wanaungana, sisi tunataka kutengana. Hiyo si sahihi lakini nguvu ya soka inaweza kusaidia kumaliza mgongano uliopo sasa kwa ina nguvu na watu wanaiamini.

Kama soka ikitumika, kutakuwa na mafanikio na hakuna atakayezuia mambo kutulia. Hata marais wan chi wataona kazi hiyo kama kweli tutaamua kufanya hivyo.
Mfano kucheza mechi za kirafiki, kusaidiana kwa karibu mambo kadhaa yakiwemo ya kiufundi.

Ufundi:
Lazima tukubali tunatakiwa kuungana ili kufanya mambo kwa uwezo wa juu zaidi. Hivyo tunaweza kuwa tunabadilishana hata walimu au wakurugenzi wa ufundi. Wa Kenya aende Tanzania na wengine hivyohivyo, lengo ni kujifunza wengine wanafanya nini.
Hakuna maendeleo ya mtu mmoja, lazima ushirikiane na watu ili ufanikiwe, ninaamini kama tuliamua tunaweza kabisa.

Migogoro:
Tukikata mpira uwe na nguvu zaidi, lazima tuondoe migogoro isiyokuwa na lazima. Angalia hapa Kenya hadi tulikuwa na ligina vyama viwili, nimepambana kwa miaka saba kulimaliza suala hilo lililodumu kwa takribani miaka 10.

Haikuwa kazi lahisi, lakini mwisho tuliamua kufanya uchaguzi wa kila ambaye angekuwa tayari kugombea. Mwisho mshindi akapatikana na hakukuwa na malumbano na sasa watu wanasaidiana.

Aminika:
Kumaliza matatizo yetu kumetufanya tuwe tunaaminika, sasa Caf inawasiliana nasi kwa ukaribu na tumeanza kufanya mambo ya maendeleo ili kubadili mambo. Angalia Gor Mahia na AFC Leopards zimerudi na mpira wa Kenya umeanza kukua kwa kasi tena.
Timu yetu ya taifa katika kipindi cha migogoro ilikuwa chini sana, lakini sasa utaona kuna mabadiliko makubwa na hata wachezaji wanaocheza Ulaya hutamani kuja, wanauliza kila mara kama wataitwa.

Kocha:
Nilijua kocha boraa nahitajika kutuvusha, kweli ikawezekana na tumempata Adel Amrouche, ikiwezekana tutamuongezea mkataba wa miaka mitano kama itawezekana.
Hadi sasa anafanya kazi yake vizuri sana na tumeridhishwa na hilo. Tunataka kufanya vizuri na kuna mipago imara tumekuwa tukifanya.

Ligi:
NAsikia kwenu Tanzania mna ligi mbili tu, ligi kuu na daraja la kwanza. Hapa Kenya tuko hadi na nne au tano hivi. Lakini katika wilaya zote 200 za Kenya mpira unachezwa na mashindano hayo yanafuatiliwa kwa karibu na KFF.

Bado tuna mipango madhubuti ya kina dada na wanawake na wenye timu zao zinafanyiwa maandalizi makubwa ili kuwa na soka bora na la uhakika kwa wanawake.

Serikali:
MWanzo nimeanza kuzungumzia kwamba tunaweza kuzisaidia serikali kutatua mgogoro huo kupitia mpira, lakini sasa nazishauri serikali za Afrika MAshariki kujenga utamaduni wa kuzisaidia klabu na hasa zinazofuzu katika michuano ya kimataifa.

Hatuwezi kushindana na Magharibi wakati zimekuwa zikipata msaada mkubwa kutoka katika serikali zaidi ambazo zina uhakika wa misaada hiyo, wakati mpira wa Afrika Mashariki unajiendesha wenyewe.
Sisi kama KFF na bodi ya ligi, kwa pamoja tumejipanga sana kuendeleza soka nchini, lakini bado tunahitaji usaidizi kutokana serikali.

Kuna mambo mengi ya kufanya lakini muda unahotajika ili kupata maendeleo hayo. Kikubwa ni kuendelea kujituma na kutoamini tulipo panatosha.

 SOURCE: CHAMPIONI NEWSPAPER


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic