November 11, 2013


Kocha wa zamani wa Simba, Patrick Liewig ametua salama kwao Ufaransa na kutaka uongozi wa Simba ummalizie fedha zake.


Liewig amesema pamoja na malipo yote, amebaki anaidai Simba dola 8,500 ambazo angependa amaliziwe kwa kuwa hana matatizo na mtu ndani ya klabu hiyo.

“Nasikitishwa na mambo yanavyokwenda, kweli sipendi kuonekana ni mkorofi au mlalamishi.
“Ukweli ninahitaji fedha zangu, halafu sitamsumbua mtu. Hivyo wanisaidie na kunilipa kila kitu.

“Nimekata tamaa Rage (mwenyekiti Simba), amekuwa akinipa ahadi mara nyingi lakini ananikwepa. Basi wanilipe tu ili niondoke kwa amani,” alisema.


Kocha huyo alikuwa nchini kwa ajili ya kudai fedha zake huku akilalama kuzungushwa na uongozi wa Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic