November 9, 2013

NYILAWILA MAZOEZINI

Bondia Kalama Nyilawila atapanda ulingoni kesho Jumapili, kwenye Ukumbi wa Zulu Paradise, Pugu Kilumba kupambana na Kaminja Ramahani.


Pambano hilo linalosubiliwa kwa hamu litakuwa ni la raundi sita na tayari kila bondia ametamba kushinda.

Pia kutakuwa na mapambano ya utangulizi kama lile kati ya Shabani Kaoneka 'BSS' na Said Mbelwa 'Moto wa Gesi' awajaoneshana kazi katika mpambano wao wa raundi nane. 

Akizungumzia Mratibu wa pambano hilo,  Rajabu Mhamila 'Super D' amesema pambano hilo ni mahususi kwa wakazi wa vitongoji vya Pugu ,Chanika,Ilala na jiji la Dar es salaam kwa ujumla 

Mapambano mengine ambayo pia ni makali ni kati ya Chirambo Hemed atavaana na Sharif Mzezele huku Adamu Ngange akioneshana kazi na Shabani Mtengela 'Zunga Boy'.

Hamza Mchanjo atamenyana na Tonny King, Twalibu Mchanjo atazichapa na Mohamed Kashinde,Said Uwezo na Sindano Paul.

Pamoja na mapambano hayo, Super D amesema uizwaji wa  DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile 
Manny Paquaio, Saul 'Canelo' Alverez ,Floyd Mayweather, Mike Tyson, Mohamed Ali na wengine kibao zitaendelea kuuzwa.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic