November 27, 2013





Beki mkongwe, Rio Ferdnand ame twitt na kueleza walivyonusurika na ajali ya ndege jana wakati wakitua Ujerumani kuivaa Bayer Leverkusen katika Ligi ya mabingwa leo.


Kikosi cha Manchester United kinachoongozwa na Kocha David Moyes kimenusurika na ajali ya ndege nchini Ujerumani.


Wakati ndege iliyowabeba Manchester United ikitua kwenye uwanja wa ndege we Cologne, mara rubani aligundua kuna ndege nyingine waliyokuwa wanakwenda kuigonga.


Haraka aliinua juu tena ili kuikwepa iliyokuwa chini na kwenda kutua mbele ya eneo walilotakiwa kutua mbele.


Kutokana na kasi hiyo wachezaji na maofisa wengine waliokuwa kwenye ndege hiyo walianguka kwenye viti.

Hali hiyo ilisababisha hofu kubwa ndani ya ndege hiyo, baada ya kutua rubani pamoja na uongozi wa shirika hilo la ndege uliomba radhi.

Manchester iliwahi kupata ajali ya ndege mwaka 1958 na kusababisha vifo vya wachezaji kadhaa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic