Kocha
Patrick Liewig amesema uongozi wa Simba umemlika dola 7,000.
Liewig
raia wa Ufaransa ambaye anadai dola 16,000 amesema amelipwa dola 7,000 na si
10,000 kama ambavyo imekuwa ikielezwa.
“Nimelipwa
dola 7,000 leo mchana, lakini wameniahidi wanaendelea kukusanya na watanilipa
nyingine 3,000.
“Naendelea
kusubiri kwa kuwa ahadi ilikuwa walipe dola 10,000 na nyingine 6,000 watanilipa
siku nyingine kulingana na makubaliano.
“Niko
hapa ila siwezi kusema ni wapi naendelea kusubiri waje kunilipa kiasi
kilichobaki. Baada ya hapo nitaondoka,” alisema.
Awali
Simba ilimlipa Liewig dola 10,000 kati ya dola 26,000 alizokuwa anadai klabu
hiyo baada ya kumvunjia mkataba na kuahidi kumlipa kiasi kilichobaki mwezi
uliopita.
Liewig
alikuwa anadai malimbikizo ya mishahara ya miezi miwili, dola 12,000 na dola
12,000 za kuvunjiwa Mkataba wakati dola 2,000 ni za tiketi yake ya kurejea
kwake.
Liewig alichukua nafasi ya Milovan Cirkovic na baada ya nusu msimu naye akatupiwa virago na nafasi kwenda kwa Abdallah Kibadeni.
Liewig alichukua nafasi ya Milovan Cirkovic na baada ya nusu msimu naye akatupiwa virago na nafasi kwenda kwa Abdallah Kibadeni.
huu ubabaishaji simba utaisha lini, rage juzi tu umechukua million 300 utoka azam TV embu mlipe lewing mbaki na makocha wenu kina kibadeni wa uswahilini,...inakera sana
ReplyDelete