November 17, 2013



AWADHI JUMA (KULIA) WAKATI AKIWA MTIBWA SUGAR AKIWA JUMA ABDUL WA YANGA MIEZI MICHACHE ILIYOPITA BAADA YA MECHI YA LIGI KUU BARA MZUNGUKO WA KWANZA KWENYE UWANJA WA TAIFA.
 Simba ambayo bado haijakaa vizuri kwenye Ligi Kuu Bara, leo imefanikiwa kuongeza nguvu kwa kusaini wachezaji wawili, Awadh Juma Issa na Ally Badru Ally.

Issa ni kiungo aliyekuwa anakipiga Mtibwa Sugar wakati Badru ni mshambuliaji aliyewahi kukipiga nchini Misri katika timu ya Canal Suez iliyokuwa inashiriki ligi daraja la kwanza hadi ilipopanda ligi kuu msimu huu, ingawa hakufanikiwa kucheza hata mechi moja.

Wawili hao wote ni wachezaji walio katika kikosi cha Zanzibar Heroes kitakachoshiriki michuano ya Chalenji nchini Kenya kuanzia Novemba 27.

Mara baada ya kutua jijini Dar na kusaini mkataba huo nyumbani kwa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage waliondoka na kurejea Zanzibar.

Awali Simba ilikuwa ikifanya mchakato wa kupata kiungo na Hassan Saleh Dilunga alikuwa kwenye target zao kabla ya Yanga kumyakua njiani.

Tayari Yanga imesajili wachezaji wawili, Juma Kaseja na Dilunga kwa ajili ya dirisha dogo lakini Simba nao wamejibu leo kwa kuwasajili wawili hao

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic