Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetuma waraka kwa
vyama vya mpira wa miguu vya wilaya, mikoa na vyama shiriki kuvitaka
kuwasilisha orodha ya wote waliofaidika na msamaha wa Oktoba 28 mwaka huu.
Oktoba 28 mwaka huu wakati akizungumza katika Mkutano Mkuu baada
ya uchaguzi, Rais mpya wa TFF, Jamal Malinzi alitoa msamaha kwa wote
waliofungiwa kwa sababu mbalimbali.
Hata hivyo, msamaha huo hauwahusu waliofungiwa kutokana na makosa
ya rushwa au kupanga matokeo. Vilevile haugusi adhabu zilizotolewa ndani ya
klabu.
Vyama vya mikoa vinatakiwa kuhakikisha waraka huo unafika kwa
wanachama wao (vyama vya mpira wa miguu vya wilaya). TFF inataka orodha ya wote
waliofaidika na msamaha huo kwa ajili ya kumbukumbu zake (records).
0 COMMENTS:
Post a Comment