November 22, 2013





Aliyekuwa kocha mkuu wa Tanzania Prisons, Jumanne Chale ameibuka na kusema kuwa ameamua kuachana na soka kwa sasa na badala yake amegeukia biashara zake mpaka hapo baadaye.
 
Chale alitimuliwa Prisons kabla ya msimu huu kufikia katikati kufuatia timu hiyo kufanya vibaya katika mechi zake kadhaa za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara.

Chale amesema kwa sasa hafikirii masuala ya mpira na amepumzika kwa kuanzisha biashara zake na mambo mengine madogo-madogo.

“Kwa sasa nipo nyumbani nimepumzika na wala sifikirii suala la soka labda hadi msimu utakapoisha ndipo nifikirie kujiunga na timu nyingine. Kwa sasa nafanya biashara zangu na mambo mengine ya kimaisha,” alisema Chale. 
SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic