Baraza la wadhamini la Simba limesema
linaendelea kumtambua Ismail Aden Rage kama mwenyekiti.
Rage bado yuko nchini Sudan na anatarajia kurejea kesho nchini na moja kwa moja atazungumza na waandishi wa habari.
Lakini mmoja wajumbe wa Baraza hilo,
Hamis Kilomoni ameonekana kujikanyaka kujibu maswali kuhusiana na uamuzi wao.
Hata hivyo baraza hilo lilikutana na wajumbe wawili tu ambao ni Kilomoni na mwenzake Ramesh Patel
SALEHJEMBE: Labda mnahisi kamati
utendaji imekosea katika kumsimamisha?
KILOMONI: Ndiyo maana hawajafuata
katiba.
SALEHJEMBE: Labda kipengele kipi unaweza
kufafanua?
KILOMONI: Aaah, hadi nisome? Ila lengo
letu ni kusuluhisha hili jambo.
SALEHJEMBE: Kama ni kusuluhisha vipi
tayari mmeingia na maamuzi yenu tayari kwamba mnamtambua Rage ni mwenyekiti.
KILOMONI: Kweli shida yetu ni
kuwakutanisha pande zote hizi mbili baada ya Rage kufika kesho (Ijumaa jioni).
SALEHJEMBE: Katiba inawaruhusu kuingilia
masuala ya kiutendaji?
KILOMONI: Hapana haituruhusu lakini sisi
pia ni wazee na kama tuna tatizo unataka tuliache tu?
SALEHJEMBE: kweli hamsitahili kuliacha,
lakini sasa Simba haina baraza la wazee, sasa nyie mnasimama upande upi?
KILOMONI: Kweli hatuna baraza na
litaundwa hivi karibuni, lakini bado sisi ni wazee. Tunaenda kama wazee.
SALEHJEMBE: Naona kama unajichanganya
Mzee Kilomoni, mara kama wadhamini mara kama wazee, kipi hasa sahihi na vipi
mmetengua uamuzi wa kamati ya utendaji.
KILOMONI: Nimekuambia wamejiuka katiba.
SALEHJEMBE: Sawa, lakini ibara au kipengele
kipi?
KILOMONI: Nimesema nimesahau hadi nijisomee
tena, au nenda katafute mwenye katiba ya Simba. Kwaheri.
SALEHJEMBE: eeh!
0 COMMENTS:
Post a Comment