November 21, 2013





Kikao kilichopangwa kufanyika kwenye makao makuu ya Simba kimekwama baada ya Kaimu mwenyekiti wa klabu hiyo, Joseph Itang’are ‘Mzee Kinesi’ kuingia uoga.
 
Mzee Kinesi ameingia uoga na kushindwa kufanya kikao hicho na waandishi walikuwa kibao wakimsubiri.
“Mzee Kinesi alisema amekwama kwenye foleni,” alieleza mwandishi wa gazeti moja.

Hata hivyo haikujulikana Mzee Kinesi alikuwa anataka kuzungumza kitu gani.
Lakini taarifa za uhakika zilieleza kwamba Mzee Kinesi alihofia wanachama kibao waliojitokeza klabuni hapo.
“Mzee Kinesi kawaambia waandishi waende kikao kikafanyike kwa mmoja wa wazee wa baraza la wazee, Mzee Kilomoni,” alisema mwandishi mwingine wa runinga.
Tayari kikao hicho cha waandishi kimeanza nyumbani kwa Mzee Kilomoni jijini Dar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic