November 27, 2013





Kipa mpya wa Yanga, Juma Kaseja, ameonyesha nidhamu ya hali ya juu kwa kufika katika siku ya kwanza ya mazoezi ya timu hiyo, lakini akapigwa ‘stop’ kuanza kazi katika timu hiyo.


Nassoro Matuzya, ambaye ni Daktari Mkuu wa Yanga, amesema Kaseja hataweza kuanza kazi rasmi wiki hii kutokana na tatizo la maumivu ya kifundo cha mguu wake wa kulia.

Matuzya amesema kipa huyo aliyesajiliwa katika kipindi hiki cha dirisha dogo tayari ameshaanza matibabu ya tatizo hilo wiki moja iliyopita ambapo sasa yuko katika wiki ya pili ya tiba hiyo na kuongeza kuwa sasa ataanza rasmi kazi yake hiyo mapema wiki ijayo.

“Tumefurahi kuona amefika katika siku ya kwanza ile jana (juzi), lakini hataweza kuanza kazi, tumemzuia kutokana na haya maumivu yake ya kifundo cha mguu ingawa ameshaanza tiba wiki moja iliyopita,” alisema Matuzya huku akiongeza kwa kusema:

“Wiki hii yupo katika wiki ya pili ya tiba hiyo ambayo inatakiwa aifanye kwa wiki mbili, nafikiri kwa hali nilivyoiona ataweza kuanza kazi rasmi wiki ijayo, kama kila kitu kitakuwa sawa kama hali inavyokwenda sasa.”

Kaseja alipata maumivu hayo wakati akifanya mazoezi yake binafsi katika kujiweka sawa kabla ya kuanza kuitumikia timu hiyo.

Kabla ya kujiunga na Yanga Kaseja alikuwa nje kwa nusu msimu baada ya kumaliza mkataba wake na timu yake ya muda mrefu, Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic