Beki Donald Musoti amekubali kutua kujiunga
na klabu ya Simba ya Dar es Salaam.
Musoti aliyekuwa beki tegemeo wa kikosi
cha Gor Mahia ya Kenya amesema kuwa yuko tayari kutua Msimbazi.
Taarifa zinaeleza tayari kuna kiongozi wa
Simba yuko jijini Nairobi kwa ajili ya mazungumzo na Musoti.
“Niko tayari kwenda Simba, lakini ni
suala la mzungumzo, huenda leo tukakutana na kumalizana hivyo subiri kidogo,”
alisema.
Kocha Zdravok Logarusic ndiye
alitependekeza kusajiliwa kwa beki huyo aliyefanya naye kazi akiwa Gor Mahia.








0 COMMENTS:
Post a Comment