Nyota wa Simba ambao hakupata nafasi ya
kucheza katika mchezo wa kirafiki wa Nani Mtani Jembe dhidi ya Yanga sasa
wataonyesha makali yao kwenye michuano ya Mapinduzi visiwani Zanzibar.
Kocha Zdravko Logarusic amesema
atatumia michuano hiyo kuwaona wachezaji wake wengine na si kukimbilia kutwaa
Kombe la Mapinduzi.
Wachezaji ambao watapata nafasi ya
kumuonyesha walichonacho kocha huyo raia wa Croatia ni pamoja na kipa Yaw
Berko, beki wa kati Gilbert Kaze na mshambuliaji Betram Mwombeki.
Akizungumza kutoka Croatia, Logarusic
alisema hakupata nafasi ya kuwaona wachezaji hao katika mechi dhidi ya Yanga
ambayo walishinda kwa mabao 3-1, hivyo michuano hiyo itakuwa nafasi kwao.
“Nitawaachia wacheze, najua timu
ataanza nayo (Selemani) Matola ambaye ni kocha mkuu. Lakini anajua tunataka
nini.
“Nitachelewa mechi moja, baada ya hapo
nitaungana nao na ningependa kuona wanacheza. Suala la kutwaa kombe si namba
moja, badala yake nataka kujenga timu kwa ajili ya ligi kuu,” alisema
Logarusic.
Berko alishindwa kuanza katika mechi
dhidi ya Yanga kwa kuwa Ivo Mapunda alipewa nafasi, Kaze alichelewa kurejea
kutoka Burundi hivyo hakukaa hata katika benchi na Mwombeki alikosa nafasi
baada ya kushindwa kumvutia kocha huyo mazoezini.
0 COMMENTS:
Post a Comment