Mshambuliaji wa TP Mazembe ya DR Congo
alionyesha kweli maisha yake sasa ni ya juu baada ya kumwaga fedha kwa
wanamuziki wa bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’.
Ulimwengu alifanya hivyo kwenye shoo
iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live, Mbagala-Zakhem, jijini
Dar siku ya Boxing Day.
Mshambuliaji huyo wa kutegemewa wa TP
Mazembe na Taifa Stars, aliingia ukumbini hapo Saa 4:45 usiku na kuwa kivutio
kwa wapenda soka waliokuwa ukumbini.
Makeke ya mchezaji huyo yalianza pale
ulipopigwa wimbo wa ‘Mtu Pesa’ kwani aliinuka kutoka katika kiti ambacho
alikuwa amekalia na kuteremka ngazi haraka na kukimbilia jukwaani huku akiwa
amekamata pochi mkononi kisha kuwavaa wanamuziki hao na kuwamwagia noti
nyekundu tu yaani ‘minoti’.
Ilionyesha kuwa wimbo huo wa ‘Mtu
Pesa’ uliotungwa na Banza Stone ambaye kwa sasa anaitumikia bendi ya Extra
Bongo ulimkuna sana mwanasoka huyo wa kimataifa.
Mbali ya wimbo huo wa Mtu Pesa nyimbo
nyingine ambazo zilionekana kumkuna mwanasoka huyo na kushindwa kutulia katika
kiti na kucheza ni ‘Jirani’, ‘Mtaa wa kwanza’, ‘Mwana Dar es Salaam’ na ‘Kisa
cha Mpemba’.
0 COMMENTS:
Post a Comment