December 9, 2013





Kipa Juma Kaseja amekiri kukutana na ugumu wa mazoezi ya timu Yanga chini ya kocha wa makipa, Razack Siwa.
 

Kaseja ametoa kauli hiyo Alhamisi iliyopita mara baada ya kumalizika kwa mazoezi kwenye Uwanja wa Bora, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Kaseja amesema kuwa tangu ajiunge Yanga, amekuwa akikutana na mazoezi magumu ambayo ameshindwa kuyatofautisha na yale ya Simba.

Kaseja alisema anayafurahia mazoezi hayo, akiamini yatamjenga katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Nimefanya mazoezi na Yanga kwa siku nne, ni ngumu kutofautisha ya hapa na nilipotoka Simba, lakini tambua kwamba mazoezi niliyoyakuta Yanga ni magumu.

“Licha na ugumu huo, nitajitahidi kuyafanya kwa ajili ya kunijenga katika mzunguko wa pili wa ligi ili niongeze kiwango changu,” alisema Kaseja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic