Mwandishi wa gazeti la Championi, Khatim
Naheka (kushoto), akimkabidhi kocha wa makipa wa Simba, James Kisaka kiasi cha
Sh 350,000 zilizotolewa na gazeti la Championi pamoja na Mwenyekiti wa kamati
ya usajili ya Simba, Zacharia Hanspope ili kusaidia matibabu.
Kulia ni Mhariri
Kiongozi wa gazeti hilo, Saleh Ally akishuhudia tukio hilo nyumbani kwa Kisaka.
Kisaka, kipa wa zamani wa Volcano ya
Kenya amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa unaosababisha mwili wake kukosa nguvu
upande mmoja ingawa mwenyewe amesema si kupooza kama ilivyoelezwa awali.
Amekuwa akiendelea na matibabu, hata
hivyo, Kisaka alilalama kushindwa kuhimili gharama kubwa ya matibabu hivyo
kuwaomba wadau wajitokeze kumsaidia.
Championi likachukua nafasi ya kuomba
wadau wajitokeze kumsaidia lakini uamuzi ukawa ni kuanza kuwa mfano kwa kutoa
angalau kiasi cha fedha ili kuwahamasisha wadau kumsaidia Kisaka ambaye hata
kutembea, analazimika kusaidiwa.
PICHA NA WILBERT MOLANDI.
0 COMMENTS:
Post a Comment