Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba, Abdallah
Kibadeni, amenyang’anywa gari aina ya GX 110 alilopewa na uongozi wa timu hiyo
akiwa anakinoa kikosi hicho.
Kocha huyo hivi karibuni alisimamishwa
na uongozi wa timu hiyo yeye na msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, kabla
ya yeye mwenyewe kutangaza kujiuzulu kuendelea kukinoa kikosi hicho.
Tetesi zilizopo hivi sasa ni kwamba, gari
hilo anatarajiwa kupewa kocha mpya wa timu hiyo, Zdravok Logarusic, raia wa
Croatia, aliyetua jijini Dar es Salaam jana asubuhi.
Kocha huyo anatarajiwa kukabidhi gari
wakati wowote kuanzia hivi sasa, mara baada ya kukamilisha baadhi ya vitu,
ikiwemo kusaini mkataba wa kuifundisha timu hiyo.
Uongozi huo utampa kocha huyo gari hilo
kwa ajili ya matumizi ya timu na binafsi katika mizunguko yake mbalimbali
nchini.
Gari hilo analotarajiwa kupewa, awali lilikuwa
likitumiwa na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Milovan Cirkovic, raia wa
Serbia, kabla hajatimuliwa.
Alipotafutwa Kibadeni kuzungumzia hilo, alisema:
“Nimeshakabidhi kila kitu kwa Simba, sitaki kuzungumza masuala yoyote ya timu
hiyo kwa sasa.”
0 COMMENTS:
Post a Comment