December 2, 2013


Uongozi wa Simba umempa nyumba kipa mpya wa timu hiyo, Yaw Berko, maeneo ya Sinza jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukaa katika muda wote atakaoitumikia klabu hiyo.


Berko ambaye yupo nchini kwa sasa, amemalizana na uongozi wa klabu hiyo na leo Jumatatu anatarajiwa kusaini mkataba wa miezi sita kwa ajili ya kuitumikia katika mzunguko wa pili wa ligi kuu baada ya kuondolewa kwa Abel Dhaira.

Kikizungumza na Championi Jumatatu, chanzo cha habari cha kuaminika kutoka Simba, kimesema Berko atakwenda kukaa Sinza kwenye nyumba ambayo ni maalum kwa wachezaji hadi mkataba wake utakapoisha.
“Kuhusu suala la nyumba ama sehemu ya kukaa Berko, haina shida kwani Simba ina nyumba nyingi ambazo huwa tunawaweka wachezaji wetu, hivyo na yeye atapewa nyumba mojawapo kati ya hizo.


“Kwa sasa yupo kwenye mazungumzo ya mwisho na uongozi ya kuingia mkataba mpya kwani ametua ili kumalizana na uongozi kisha atarudi kwao na baadaye atarejea tena kuanza kazi,” kilisema chanzo hicho.
SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic