December 4, 2013


Siku chache baada ya timu ya Oljoro kutangaza kuwania saini ya aliyekuwa kocha wa Coastal Union, Hemed Morocco, hatimaye kocha huyo amekubali kusaini mwaka mmoja kukinoa kikosi hicho.


Morocco amesema anatarajia kuripoti rasmi kambini leo huku akisema suala la kwanza litakuwa ni kuimarisha kikosi hicho kwa kufanya usajili baada ya uongozi wa Oljoro kumpa jukumu hilo kwa kile walichosema wana imani naye kama kocha mwenye uzoefu mkubwa na Ligi Kuu Bara.

Aidha, pamoja na kupewa jukumu la usajili, Morocco alipata hofu kwamba haitakuwa kazi rahisi kwake, kwani hafahamu uwezo wa wachezaji wake kwa kuwa kikosi hicho kilimaliza katika nafasi mbaya (nafasi ya 10) kwenye mzunguko wa kwanza.


“Kawaida yangu huwa nasaini mwaka mmoja. Natarajia kuripoti Jumatano (leo) na sitakuwa na muda wa kupoteza kwani kazi ya usajili itaanza mara moja, hivyo nitafute kuanzia kesho nitakuwa na jibu la nani ataongezwa kikosini,” alisema Morocco huku akikiri kuwa haitakuwa kazi rahisi kukibakiza ligi kuu kikosi hicho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic