December 2, 2013


Kipa Juma Kaseja leo ameanza rasmi kuitumikia Yanga ambayo ameingia nayo mkataba wa miaka miwili.

Kaseja ameanza mazoezi leo kwenye Uwanja wa Bora Kijitonyama jijini Dar es Salaam na kuwa kivutio kwa wengi waliohudhuria mazoezi hayo.


Kipa huyo wa zamani wa Simba, amekutana na Ally Mustapha ‘Barthez’ aliyekuwa kipa msaidizi wake walipokuwa Simba.

Wakati fulani Barthez aliwahi kulalamika kwamba hakuwa akipata nafasi ya kudaka kwa kuwa Kaseja alikuwa akidaka mechi zote.


Lakini Mungu si Athumani! Makipa hao wamekutana kwa mara nyingine, wakiwa nje ya mipaka ya Msimbazi, safari hii Msimbazi.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic