Siku
chache baada ya Kocha Mkuu wa Ruvu Shootings, Charles Mkwasa, kuweka wazi kuwa
amemalizana na uongozi wa klabu hiyo kutaka kuondoka, tayari Ruvu wamepanga
kumtangaza rasmi mrithi wake keshokutwa Alhamisi, ambaye atakiongoza kikosi
hicho katika raundi ya pili ya ligi kuu.
Mkwasa
amekubali kufanya kazi na mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga SC, kama
kocha msaidizi huku akichukua mikoba ya Fred Felix ‘Minziro’ ambaye hatima yake
mpaka sasa haijajulikana huku kocha mkuu Ernie Brandts akitimuliwa kazi
kutokana na mwenendo mbaya wa timu.
Msemaji
wa Ruvu, Masau Bwire, alikiri kuwa Mkwasa amefikisha barua kwa viongozi
wake hivyo wanahaha kumtafuta mrithi wake haraka iwezekanavyo.
“Ni
kweli Mkwasa, ameonesha nia ya kuondoka, tumemshauri kubaki lakini hakutaka na
tayari amewasilisha barua ya kuondoka. Kuhusu mrithi wake atatangazwa rasmi
Januari 2, siku ambayo tutaweka bayana kila kitu, likiwemo la mkataba wake,”
alisema Bwire.








0 COMMENTS:
Post a Comment