December 1, 2013



 
Timu ya Bara, Kilimanjaro Stars imepata ushindi wake wa kwanza katika michuano ya Chalenji kwenye Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi, Kenya.
 
Bao pekee katika mcheoz huo lilifungwa na Haruna Chanongo katika kipindi cha pili akiunganisha krosi safi ya Frank Domayo aliyekuwa amepewa pasi ya chini ya Ramadhani Singano ‘Messi’.

Pamoja na  Stars kujitahidi na kulishambulia mfululizo lango la Somalia lakini bado washambuliaji wake hawakuwa makini katika kufunga.

Katika mechi ya kwanza Stars ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Zambia katika uwanja wa Machakos uliokuwa umejaa tope kama wa mchangani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic