December 1, 2013





Kocha mpya wa Simba, Zdravko Logarusic amewasili nchini leo na kusema yuko tayari kwa ajili ya kuanza kazi.
 
Awali ilielezwa kocha huyo hatakuja nchini kwa kuwa Mwenyekiti wa Simba aliyesimamishwa, Ismail Aden Rage alitangaza kuwarudisha Abdallah Kibadeni na Jamhuri Kiwhelo 'Julio'. Lakini wapi bana, kocha huyo ametua Dar tayari kwa kuanza kazi.

Kocha huyo ameonyesha kweli yuko shap maana ameishakagua kiwanja cha Kinesi na mara moja ameingia katika mitaa ya Dar.
“Niko tayari kwa kazi, nataka kufanya vizuri lakini najua kuwa maandalizi ndiyo kitu muhimu.

“Lakini siwezi kusema sana kwa sasa hadi nitakapowaona wachezaji,” alisema Logarusic.

Wajumbe wa kamati ya utendaji ya Simba walijitokeza uwanjani wa ndege kumpokea wakiongozwa na Swed Nkwabi ambaye ni kaimu makamu mwenyekiti.
Wengine waliokuwepo ni Danny Manembe na Said Pamba ambao waliondoka na kocha huyo uwanjani hapo.
 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic