Kipa namba moja wa Mbeya City, David
Burhan amesema kuvaa jezi namba 18 kwake kuna maana kubwa hasa katika maisha
yake.
Mbeya City ilimsajili kipa huyo msimu
huu akitokea Tanzania Prisons ambapo ameliambia gazeti hili kuwa, namba 18
inawakilisha siku yake ya kuzaliwa na siyo jambo lingine lolote na kusisitiza
kuwa, ndiyo maana imekuwa yenye bahati kwake.
“Wengi wananiuliza kwa nini sikuchagua
jezi namba moja kwa kuwa mimi ni kipa, lakini hii ni kawaida yangu kuitumia
namba hiyo.
“Hata kwenye timu zangu za awali kabla
ya kutua Mbeya City nilikuwa nikiitumia namba hiyohiyo, ikitokea naenda sehemu
nyingine nitavaa namba hiyo pia. Nilipokuwa Polisi Iringa na Prisons kote
nilivaa namba 18,” alisema Burhan.
0 COMMENTS:
Post a Comment