Baadhi ya
wachezaji wa Mtibwa Sugar wamegomea kujiunga na wenzao mazoezini kwa madai ya
kutolipwa mshahara wa mwezi uliopita pamoja na wengine kutaka kuongezewa
mikataba.
Kikizungumza na SALEHJEMBE, chanzo cha ndani kilisema wachezaji wengi mastaa wamegomea kwa kuwa
hawajalipwa mshahara wa mwezi uliopita huku wengine wakiwa wamebakisha muda
mchache kwenye mkataba wao, hivyo wanataka kuongezewa.
“Wamegomea kuanza
mazoezi na wenzao, kuna madai mawili, mshahara wa mwezi uliopita pamoja na
wengine ambao mikataba yao inakaribia kumalizika wanataka wapewe mipya,”
kilisema chanzo hicho.
Alipotafutwa
Meneja wa Mtibwa, David Gboya, alisema: “Mshahara tunaodaiwa ni wa mwezi huu
ambao hata muda wa kulipa bado, ndiyo maana hawajaja, naona wanataka fedha za
kuziachia familia zao, wao watakapokuwa kazini, wasijali kwa hilo.”
0 COMMENTS:
Post a Comment