December 20, 2013




Timu ya ya Kagera Sugar inatarajia kucheza mechi nne za kirafiki na timu za Sports Club Villa, Express, URA na Bunamwaya kutoka Uganda ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuanza Januari, mwakani.


Kocha Msaidizi wa Kagera, Mrage Kabange amesema wameamua kucheza mechi za kirafiki na timu za Uganda kutokana na ubora wao, pia urahisi wa kuzifikia timu hizo.

“Tunaamini timu hizo zitakuwa kipimo kizuri kwetu kabla ya ligi kuu, utaratibu wa kucheza na timu hizo utaanza baada ya wiki mbili kutoka sasa.

“Timu za Uganda zina ubora unaotakiwa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati, hata wachezaji wanaotoka huko wakija huku wanafanya vizuri katika ligi yetu, maamuzi tuliyofanya ni sahihi na naamini itakuwa kipimo tosha,” alisema Mrage ambaye timu yake inashika nafasi ya tano katika msimamo wa ligi kuu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic