| WAKATI WA UHAI WAKE; KISAKA AKISAIDIWA KUVISHWA VIATU NA MWANAYE, HUKU AKIWA AMESHIKWA NA MKEWE MDOGO KWA KUWA HAKUWA AKIWEZA KUTEMBEA MWENYEWE. |
Kocha wa zamani wa makipa wa Simba,
James Kisaka ataangwa kesho Saa 9 Alasiri kabla ya kusafiriswa kwao Tanga kwa
mazishi.
Kisaka aliyefariki leo alfajiri katika
Hospitali ya Burhan, mwili wake utaangwa katika hospitali ya Muhimbili jijini
Dar.
Kisaka alikuwa amepooza upande mmoja,
ameugua kwa zaidi ya mwezi mmoja hadi alipolazwa katika hospitali hiyo.
Msemaji wa Familia, Benny Kisaka amesema
mwili wake utasafirishwa kijijini kwao mkoani Tanga kwa mazishi baada ya
kuangwa jijini Dar.
"Kwa sasa msiba uko Mbezi, ni mbele ya Mbezi kwa Msuguri nje kidogo ya jiji la Dar," alisema Kisaka ambaye ni mmoja wa waandishi waandamizi wa michezo na burudani.







0 COMMENTS:
Post a Comment