Kiungo nyota wa Simba, Abdallah Singano
‘Messi’ amepata baraka baada ya kupewa zawadi ya gari na mwanachama wa klabu
hiyo.
Mwanachama wa siku nyingi wa Simba,
Musleh Al Rawahi ambaye amekuwa karibu na klabu ya Simba tokea akiwa mtoto mwaka
1977.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Simba
zinaeleza mwanachama huyo amempa Messi gari aina ya Suzuki Carry ambalo kiungo
huyo mwenye miaka 21 analitumia kumuingizia fedha.
“Unajua Muslah ni mtu anayependa sana
maendeleo ya Simba, hivyo alivyoona Messi anajituma na ana nidhamu, akajitolea
kumpa gari.
“Aliulizwa anataka gari ya aina gani,
yeye Messi akachagua gari hiyo kwa ajili ya kubebea mizigo ili awe anaingiza
fedha.
Ameonyesha ana akili sana maana angekuwa mtu mwingine angechagua gari la kutembelea,” kilieleza chanzo cha uhakika.
Ameonyesha ana akili sana maana angekuwa mtu mwingine angechagua gari la kutembelea,” kilieleza chanzo cha uhakika.
Alipotafutwa Messi kuhusiana na hilo,
alitoa ushirikiano ingawa hakutaka kulizungumzia sana suala hilo katika vyombo
vya habari.
“Ulichosema ni kweli, Muslah ni mtu
anayependa maendeleo ya Simba, pia amewasaidia watu wengi tu. Ila mimi
niliposikia gari ndiyo nikaamua kuchagua hilo la kubeba mizigo badala ya lile
la kutembelea.
“Awali niliona kama utani, kweli imekuwa
hivyo na ninamshuru Mungu maana linaniingizia fedha kiasi. Lakini kwa kuwa
sipendi makuu, wengi hawajui hata kama nina gari, hivyo sipendi kuzungumza sana
suala hili hapa,” alisema.
Juhudi za kumpata Muslah hazikuzaa
matunda kwa kuwa ilielezwa yuko nchini Oman ambako hufanya kazi zake na
kuendesha maisha yake lakini pia hapa nchini ana kampuni zake hivyo atarejea
hivi karibuni.
Messi alionyesha uwezo mkubwa katika
mechi ya Jumamosi iliyopita wakati Simba ilipoivaa Yanga katika mechi ya Nani
Mtani Jembe na kushinda kwa mabao 3-1, kiungo huyo akiwa kati ya waliong’ara.
Alisababisha penalti baada ya kumyanyasa
beki David Luhende lakini akasababisha Kelvin Yondani apewa kati nyekundu baada
ya kumtoka naye akamfanyia faulo na kupewa kadi ya pili ya njano iliyozaa
nyekundu.
0 COMMENTS:
Post a Comment