Kocha Mkuu wa Kenya, Harambee Stars,
Adel Amrouche amesema mechi ya nusu fainali ya Kombe la Chalenji kati ya kikosi
chake itakuwa ngumu.
Amrouche raia wa Ubelgiji mwenye asili
ya Algeria amesema mechi itakuwa ngumu sana na kila timu italazimika kufanya
kazi ya ziada.
“Kazi ni ngumu sana katika mechi hiyo,
tunawaheshimu Tanzania lakini tunachotaka ni kushinda nyumbani.
“Tunataka kufanya vizuri na kubakiza
kombe nyumbani, mechi dhidi ya Taifa Stars haitakuwa lelemama,” alisema
Amrouche.
Kocha huyo ni kati ya wale wanaopewa
sifa kubwa kutokana na soka la pasi na kasi na pia anajulikana kwa kuwa na
mipango ya ushindi.
Wakati akiwa Kocha wa timu ya taifa ya
Burundi, aliiongoza timu hiyo kuvifunga vigogo kadhaa kama Misri na Ivory
Coast.







0 COMMENTS:
Post a Comment