Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts amesema kipa wake
mpya, Juma Kaseja si kipa namba moja.
Brandts amesema Kaseja ni kipa mzuri na mzoefu
lakini hana uhakika wa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza hadi
atakapoonyesha juhudi mazoezini.
“Akionyesha juhudi sawa, tutampa nafasi ya kucheza
kama kipa wa kwanza.
“Lakini akipata nafasi hiyo, pia lazima aonyeshe
uwezo kuishikilia.
“Hauwezi kusema kipa fulani ndiyo namba moja kwa
kuangalia jina lake tu, si sahihi,” alisema.
Kaseja amejiunga na Yanga, baada ya Simba kumuacha kwa
madai kuwa kiwango kimeshuka, hata hivyo haikuwa sahihi.
0 COMMENTS:
Post a Comment