December 7, 2013


Kocha wa makipa wa Simba, James Kisaka ameshukuru watu kadhaa waliojitokeza kumsaidia na kumjulia hali.
 “Nafarijika sana kuona watu wananitafuta na kunijulia hali, ndani ya jana na leo naona watu wengi wamenitafuta.

“Unajua mtu akikujua hali tu inatia moyo sana, nasikia raha kwa kweli na ninaona watu wananijali,” alisema.
Kisaka amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa unaosababisha kukosa nguvu upande mmoja wa mwili.
Lakini mwenyewe amekuwa akisisitiza kuwa si kupooza, badala yake ni ugonjwa ambao bado hajaambiwa ni upi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic