Na
Saleh Ally
MECHI
ya kesho ya kirafiki ya Nani Mtani Jembe kati ya watani Simba na Yanga kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ina mambo mengi.
Burudani
ya mchezo wa kesho inaonekana zaidi imetekwa na mshambuliaji wa zamani wa Simba
na mpya Yanga, Emmanuel Okwi ambaye anarudi tena katika mechi ya watani, akiwa
upande wa Yanga.
Watakaokwenda
uwanjani, wengi watataka kuwa mashahidi wa mawazo yao kwamba kweli Okwi anaweza
kuichezea Yanga? Kesho atakuwa kwenye namba 25 lakini safari hii ni njano na
kijani na si nyekundu na nyeupe.
Katika
soka, yote yanawezekana lakini kikubwa ni kupata uhakika na kuwa shahidi wa
macho, kuhakikisha kama kweli kimetokea.
Mambo
mengi yanayovutia kwa Okwi hiyo kesho ni kwamba mechi yake ya mwisho ilikuwa ni
Mei 6, 2012 Simba ilipoifunga Yanga kwa mabao 5-0 kwenye uwanja huohuo wa Taifa
jijini Dar es Salaam.
Baada
ya hapo, mzunguko wa pili hakucheza kwa kuwa alikuwa na kadi nyekundu
aliyoipata katika mechi dhidi ya JKT, baada ya hapo wakati Simba ikienda kupiga
kambi nchini Oman kwa ajili ya kujiandaa na mzunguko wa pili chini ya Patrick
Liewig, yeye ‘akauzwa’ Etoile du Sahel ya Tunisia.
Katika
mechi ya ushindi wa mabao 5-0, Okwi alifunga mabao mawili, akasababisha mawili
na sasa anarudi kuichezea Yanga. Swali, atasababisha au kufunga mangapi?
Kocha
Ernie Brandts haitakuwa rahisi kumuanzisha, kwa kocha wa kiwango chake lazima
ataangalia suala la ugeni wake katika kikosi, atamuanzisha benchi na kumuingiza
hapo baadaye.
Akiingia
atafanya nini? Ndiyo swali. Soka lina mambo mengi, huenda akaingia na
kushangaza kwa kufanya makubwa kama kawaida yake, lakini inawezekana pia
akadoda kwa kuwa anahitaji muda, yote yanawezekana.
Nani
atamkaba?
Kama
Kocha Brandts atamuingiza Okwi, mfano kuchukua nafasi ya Simon Msuva, beki yupi
atakuwa na uwezo wa kutosha kumzuia? Kweli katika soka kila kitu kinawezekana.
Mfano
mzuri wa makali ya Okwi, mkongwe Shadrack Nsajigwa angekuwa na jibu, lakini
sasa huenda mzigo ukamuangukia Said Nassor ‘Chollo’ au Issa Rashid ‘Baba Ubaya’
kulingana na Zdravko Logarusic atakavyopanga kikosi. Itakuwaje? Vizuri
kusubiri.
Pasi
za uhakika?
Wakati
Okwi aking’ara alikuwa amezungukwa na viungo mahiri wenye uwezo wa juu sana.
Angalia Haruna Moshi ‘Boban’, Mwinyi Kazimoto na marehemu Patrick Mutesa
Mafisango. Swali, Yanga kuna watu wenye uwezo wa kazi hiyo?
Inawezekana
pasi za Athumani Iddi ‘Chuji’ au Frank Domayo zikawa msaada mkubwa kwake.
Haruna Niyonzima pia anaweza kuwa hivyo, hasa kama ataachia mpira mapema kwa
Okwi.
Anakutana
nao:
Okwi
anakutana tena na Juma Kaseja, Ally Mustapha ‘Barthez’ (kama atakuwa katika
listi) na Kelvin Yondani ambao alikuwa nao katika kikosi kile kilichoshinda
5-0.
Wao
watatu au wanne wanaweza kuisaidia Yanga kulipa kisasi kesho? Majibu ya mpira
ni baada ya dakika 90, kwani Simba pia inaweza kushinda na kuwashangaza ambao
hawafikirii hivyo.
Berko
tena?
Wakati
Yanga inalala kwa mabao 5-0, Okwi alifunga bao ‘baya’ la kwanza baada ya
kuwapita mabeki watatu na kuingia nao kabla ya kupiga shuti lililompita kipa
Mghana, Yaw Berko.
Leo
Berko yuko Simba, hakuna ujanja lazima atakuwa langoni au katika benchi. Kama
akianza maana yake atakuwa amekutana na Okwi tena baada ya miezi 15, ataweza
kumzuia asitikise tena nyavu zake?
Hatari:
Huenda
Hamis Kiiza akawa hatari zaidi kesho kwa Simba, licha ya kuwa, amekuwa
akiwafunga mara nyingi lakini safari hii atasaidiana na Okwi ambaye amecheza
naye mechi nyingi wakiwa timu ya taifa ya Uganda, The Cranes.
Okwi
anajua Kiiza anataka nini, hali kadhalika Kiiza anajua Okwi anataka nini. Hivyo
mabeki wa Simba wanapaswa kuwa makini na huenda Joseph Owino akawa msaada
mkubwa kwa wenzake kwa kuwa pia anaijua vizuri kazi ya wawili hao wakati akiwa
URA au wanapokutana The Cranes.
Mabadiliko:
Mashabiki
leo wana kazi ya kubadili mambo, Mei 6, 2012, mashabiki wa Simba walimshangilia
sana Okwi kuliko siku nyingine. Huenda leo wakafanya kazi kubwa ya kumzomea.
Mpira
ni burudani ya aina yake, kwani hata mashabiki wa Yanga ambao walimzomea Okwi
kwelikweli, nao watakuwa wakimshangilia utafikiri wanamuona kwa mara ya kwanza
na hawakuwahi kumzomea hata kidogo.
Huenda
ndiyo mapenzi ya dhati lakini ukweli ni kwamba wanampokea na kumsisitiza au
kumshawishi kwamba na wao wanataka 5-0.
Ingawa
timu hizo zilikutana mara mbili baada ya mechi hiyo, lakini bado mechi ya 5-0
ndiyo imekuwa gumzo zaidi. Kama ukiiangalia mechi hiyo, watakaokosekana leo katika
kila timu ni hawa wafuatao:
Watakaokosekana
Simba:
Juma
Kaseja
Ally
Mustapha ‘Barthez’
Amir
Maftah
Shomari
Kapombe
Mwinyi
Kazimoto
Haruna
Moshi ‘Boban’
Mutesa
Mafisango (marehemu)
Felix
Sunzu
Emmanuel
Okwi
Watakaokosekana
Yanga:
Yaw
Berko
Shadrack
Nsajigwa
Juma
Seif ‘Kijiko’
Nurdin
Bakari
Rashid
Gumbo
Davis
Mwape
Kenneth
Asamoah
FIN.
0 COMMENTS:
Post a Comment