December 11, 2013


KOKE AKICHUANA NA MESSI


Na Saleh Ally
Pamoja na Ligi Kuu England kupewa sifa ya ugumu zaidi, lakini inaonekana kuna ligi ambazo zina ufundi mwingi zaidi kuliko hiyo ya England.
 
Hispania ‘La Liga’ wamekuwa wakipewa sifa kubwa ya uchezaji na timu zao ndiyo zinaongoza kwa umiliki wa mpira na pasi za burudani.
Mfano Barcelona, ndiyo timu yenye uwezo mkubwa wa kumiliki mpira huku ikipanga mashambulizi bila ya kuupoteza kwa kipindi kirefu zaidi.

Hata kama mabao ni muhimu, lakini pasi za uhakika ni burudani ambayo huwavutia mashabiki wengi wa soka duniani kote.

Kwa hapa nyumbani, Simba ndiyo imekuwa ikipewa sifa ya timu inayopiga pasi nyingi na fupifupi ingawa katika siku za karibuni inaonekana kupoteza sifa hiyo na kuwa na kikosi ambacho hata mashabiki wake hawakiamini kama ilivyokuwa hapo awali.

Mabao ni burudani ya uhakika, pasi zinavutia pia mashabiki wengi lakini pasi zinazozaa mabao ndiyo kipenzi cha makocha wengi wa soka.
Kila kocha anataka kuwa na mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kupiga pasi za mwisho zinazozaa mabao na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi, maana timu ili ishinde lazima ifunge na kuzuia kufungwa.

Ili ifunge, lazima pasi ya kusababisha bao ipatikane. Hayo ni mafunzo na uwezo wa mchezaji binafsi na inaonekana wachezaji wengi wa aina hivyo wanaishi Hispania inapochezwa La Liga.

Wachezaji hao wako La Liga bila ya kujali uraia wao ni nchi gani na katika takwimu za wapiga pasi mahiri zilizotolewa wiki iliyopita, zinaonyesha wachezaji wengi wanaokipiga katika ligi hiyo ya Hispania ndiyo wakali.

Wachezaji kutoka England yaani Premiership wameachwa mbali na wakali kutoka Hispania na hata wale wa Ujerumani, Bundesliga.
Ukichukua tano bora ya Ulaya ya wapigaji bora wa pasi za mwisho, hukuti hata mchezaji mmoja kutoka England. Kwani watatu wa juu wote wametoa pasi nane zilizozaa mabao na wanatokea Hispania.

Wakali hao wenye pasi nane ni Koke wa Atletico, Cesc Fabregas na Neymar (wote Barcelona). Halafu wanafuatia wenye pasi sana ambao wote wanatokea Ujerumani ambao ni Gonzalo Castro wa Bayer Leverkusen na mchezaji bora Ulaya, Frank Ribery wa Bayern.
Hakuna mchezaji hata moja wa England aliyeingia katika kikosi hicho cha tano bora cha kina ‘master’ wa kupiga pasi kwa kuwa mtu wa kwanza kwa pasi za mabao England ni Steven Gerrard wa Liverpool.

Gerrard ana pasi sita sawa na Mesut Ozil wa Arsenal ambaye alikuwa mchezaji wa Real Madrid kabla ya kutua mitaa ya Emirates msimu huu.
Wengine wanaounda tano bora ya wapiga pasi England ni Wayne Rooney (Man United), Aaron Ramsey (Arsenal) na Kevin Mirallas wa Everton.

Ukiangalia kwa England kwa kiasi kikubwa utaona kweli utoaji pasi za mwisho, zaidi unategemea kipaji cha mchezaji husika.
Angalia Man United, bado inayumba kukwea kileleni lakini kwa kiasi kikubwa Rooney amekuwa akiendelea kufanya vizuri na kuonyesha kiwango kikubwa.
Lakini hata Koke wa Atletico anayeongoza Ulaya, timu yake siyo inayofanya vizuri kuliko Barcelona, Madrid na Atletico Madrid lakini kwa uwezo wake, ameendelea kufanya vizuri zaidi.

WAKALI ULAYA
                                           TIMU           PASI
        Atletico
8
        Barcelona
8
        Barcelona
8
        Leverkusen
7
        Bayern
7

























     
WAKALI ENGLAND


   TIMU
  PASI

   Liverpool
6

    Arsenal
6

    Man United
5

     Arsenal
5

     Everton
5

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic