Kocha Mkuu wa Simba, Zdravok Logarusic,
amesema anahitaji mechi mbili zaidi zikiwa ni dakika 180 ili kuweza kukipima
kikosi chake kabla ya mechi yao ya Mtani Jembe dhidi ya Yanga.
Mechi ya Mtani Jembe inatarajiwa kupigwa
Desemba 21 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Logarusic amepewa mkataba wa miezi sita
wa kuitumikia Simba baada ya kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Abdallah
Kibadeni.
Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala,
amesema kocha huyo tayari ameshakiona kikosi na kusema kuwa anataka mechi mbili
kabla ya kuivaa Yanga.
“Tutacheza na KMKM lakini kocha
amehitaji mechi nyingine zaidi ambapo tutacheza mbili kabla ya kuivaa Yanga.
“Lengo la kocha ni kuangalia uwezo wa
kila mchezaji ili aweze kuona viwango vyao na kuweza kupanga timu. Tayari
ameshawaona kwenye mazoezi na sasa anataka awaone jinsi wanavyocheza kwenye
mechi,” alisema Mtawala.
Hii ina maana kuwa, kocha huyo atatumia
dakika 180 uwanjani ili kujua ni jinsi gani timu yake inaweza kuisambaratisha
Yanga.
SOURCE: CHAMPIONI







0 COMMENTS:
Post a Comment