December 22, 2013



 
MANJI AKIZUNGUMZA LEO NA WAANDISHI WA HABARI, KUSHOTO NI MAKAMU MWENYEKITI CLEMENT SANGA AMBAYE ANAKAIMU UENYEKITI KUTOKANA NA SAFARI YA MANJI NJE YA NCHI.
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amesema kama ni lawama za kufungwa yakiwemo makosa ya kipa Juma Kaseja mzigo aangushiwe yeye.


Pamoja na hivyo, Manji aliwapongeza Simba kutokana na kucheza vizuri na kushinda mchezo wa juzi, huku akisisitiza Yanga hawana sababu ya kulumbana kwa kuwa ulikuwa ni mchezo wa fete au bonanza.


Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo kwenye makao makuu ya klabu hiyo jijini Dar es Salaam, Manji alisema hakuna haja ya kumtupia lawama Kaseja wala mchezaji mwingine kutokana na kipigo cha mabao 3-1 katika mechi ya Nani Mtani Jembe, juzi.

“Ninaomba mimi ndiyo nipiwe lawama hizo zote na kama kuwajibika basi niwe mimi, pia Kaseja aachwe naomba hakuna chochote kibaya alichokifanya, kama ni makosa yote yalikuwa ya kimchezo.


“Naomba niwaondoe hofu mashabiki kuwa wapinzani wetu hawatatufunga tena katika kipindi chote nitakachokuwepo madarakani kwa kuwa hii ni mara ya kwanza Yanga inapoteza kwa Simba mimi nikiwa mwenyekiti.

“Ushindi wa Simba ni katika mechi ya fete au bonanza, hivyo hatupaswi kuchanganyikiwa na angalia hadi leo tunaongoza ligi,” alisema Manji aliyesema anayeondoka leo nchini na kuacha madaraka kwa makamu wake, Clement Sanga.

“Hivyo nawaomba tuwe watulivu, tuamini tunaweza kujirekebisha na kuendelea kufanya vizuri. Pia watendaji wa Yanga waendelee kupambana kurekebisha mambo.

Pamoja na hivyo, Manji alimchambua mwanachama mmoja kwa kumlaumu hadharani yeye pamoja na Kaseja.

“Kuna mzee ambaye ni mwenzetu, anailaumu Yanga kwa  kumsajiliwa Kaseja na badala yake tungemsajili Ivo Mapunda, aachane na habari zake akumbuke kuwa kipa huyo aliwahi kufungiwa miezi kwa kile kilichodaiwa kuihujumu timu tulipocheza na Simba na wakatufunga, ni vyema akatambua kuwa Kaseja ni kipa namba moja,” alisema Manji.

Manji alisisitiza Yanga bado ina kikosi imara badala yake wanatakiwa kurekebisha mambo kadhaa ili kujiimarisha zaidi.

1 COMMENTS:

  1. maneno ya mkosaji kabla ya mchi mbona hakusema bonanza. hizo ni hasira za bao tatu. duh kunbe inaumizaaa. eee6 - 0, 5 - 0 . 3 -1.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic