Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola
amesema mshambuliaji Betram Mwombeki hajawahi kufukuzwa.
Matola amesema mara nyingi imeelezwa
Mwombeki ametemwa, lakini usahihi ni kutopata na nafasi ya kucheza kutokana na
mfumo mpya wa kocha.
“Unajua kocha ameanzisha utaratibu mpya wa
wachezaji. Nitakupa kwa mfano, ameteua wachezaji 25, hiki ndiyo kikosi chake.
“Tunapokwenda kwenye mechi anaweza
kusema anataka wachezaji 20 tu, zaidi ya hapo wanapumzika. Tukirudi mazoezi nao
wanarudi.
“Baada ya kuanza maandalizi upya tena
inategemea kila mmoja anamridhisha vipi kocha na anaweza akarudi na yule
aliyekuwepo asipangwe au kuingia kwenye benchi.
“Hii si kufukuzwa badala yake ni kupanda
na kushuka katika kikosi na kila mchezaji anapaswa kujituma ili kupata nafasi,”
alisema Matola.
Hivi karibuni kulikuwa na taarifa huenda
Mwombeki ametemwa katika kikosi cha Logarusic ambaye amekuwa kocha asiyetaka
mzaha.







0 COMMENTS:
Post a Comment