Wanachama
wa Pan African wametakiwa kufuata ngazi husika pale wanapoona viongozi wa klabu
yao wanakwenda kinyume na Katiba yao.
Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imetoa mwongozo huo kwa wanachama wa Pan
African baada ya kumwandikia barua Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) kulalamikia uongozi wao wakati wao si wanachama wa TFF.
Wanachama
hao wanalalamikia uongozi wa klabu yao kwa kuitisha mkutano wa uchaguzi kabla
ya ule wa kawaida ambao unatakiwa kufanyika mara moja kwa mwaka.
Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF imelazimika kutoa mwongozo huo kwa vile
wanachama hao katika malalamiko yao wamekigusa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Dar es Salaam (DRFA) ambacho ni mwanachama wa TFF.
Pan
African ni mwanachama wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Ilala (IDFA) ambao
ndiyo wanachama wa DRFA. Hivyo, TFF imemtaka mwanachama wake DRFA kupitia IDFA
kufuatilia tatizo hilo na kulipatia ufumbuzi.







0 COMMENTS:
Post a Comment