Kocha
Msaidizi wa Yanga, Felix Minziro amemwambia aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Simba,
Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ apunguze kuzungumza, badala yake afanye kazi.
Julio
hivi karibuni alitimuliwa na Simba pamoja na aliyekuwa Kocha Mkuu, Abdallah
Kibadeni ambaye sasa ametua Ashanti United.
Minziro
amesema Julio ana uwezo mkubwa wa kufundisha, kikubwa kinachomponza ni kelele
anazozipiga kitu ambacho siyo sahihi.
“Nampa
ushauri wa bure mdogo wangu Julio, ili adumu kwenye timu zetu za Bongo muda
mrefu, basi aache kelele, badala yake afanye kazi pekee, ninaamini atafanikiwa
zaidi ya hapo alipo.
“Julio
ana uwezo mkubwa wa kufundisha soka, anaingia kwenye orodha ya makocha bora
nchini kutokana na uwezo wake mkubwa, kama akiufanyia kazi ushauri wangu,
atafika mbali,” alisema Minziro.








0 COMMENTS:
Post a Comment