Wachezaji wa Yanga wameomba kuonana na mwenyekiti wao, Yusuf Manji kwa ajili ya
mazungumzo kabla ya kumaliza muda wake baada ya kusema hana mpango wa kugombea
uongozi klabuni hapo mara baada ya muda wake wa kuwepo madarakani kumalizika.
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, alisema
hajajua sababu ya mwenyekiti huyo kutopanga kugombea tena, hivyo kwa niaba ya
wenzake ameomba wakutane kwa ajili ya kuzungumza naye masuala kadhaa.
Cannavaro
alisema mwenyekiti bado anahitajika katika timu hiyo katika kuleta maendeleo na
hasa kipindi hiki ambacho timu hiyo inajiandaa kwa mzunguko wa pili wa Ligi kuu
Bara pamoja na michuano ya kimataifa mwakani.
“Ujue
hadi hivi sasa wachezaji kinachoendelea kuhusiana na Manji kujitoa Yanga
hatukijui vizuri, kikubwa tunachokiomba ni kukutana na mwenyekiti. Ninaamini ni
kiongozi bora atakayeipa maendeleo na mafanikio timu yetu, ni vema akaendelea
kuiongoza Yanga,” alisema Cannavaro.
Straika
wa timu hiyo, Jerry Tegete, naye alisema: “Mimi sijui chochote kinachoendelea,
kikubwa nasikia amejitoa Yanga, hivyo ni vema tukakutana naye kwa ajili ya
kuzungumza naye ili kujua kinachoendelea.”







0 COMMENTS:
Post a Comment