December 30, 2013





Yanga imemjumuisha Kocha Zdravko Logarusic wa Simba katika idadi ya makocha inaowataka.
 
Habari za uhakika zimeeleza Yanga imemjadili kocha huyo na huenda ikafanya naye mazungumzo ili asitishe mkataba wake wa miezi sita Simba na kutua Jangwani.

Ingawa viongozi wa Yanga wamekuwa wagumu kulizungumzia suala la kocha mpya baada ya kumtema Ernie Brandts, lakini Logarusic ni kati yao.

“Kweli kabisa, Yanga wamevutiwa na kazi ya Logarusic na wanaamini ana uwezo wa kuwathibiti mastaa wa Yanga.

“Hivyo wamempa mtu kazi ya kuwasaidia kuzungumza naye na ikiwezekana mara moja ajiunge na timu hiyo.

“Unaweza ukasikia wakati wowote amechukuliwa na kuanza kuifundisha timu hiyo,” kilieleza chanzo cha uhakika.
Juhudi za kumsaka Logarusic akiwa nchini kwao Croatia kwa ajili ya mazungumzo zilifanikiwa na alisema hivi:
“Naiheshimu Yanga, lakini naheshimu zaidi mkataba wangu wa miezi sita na Simba, sasa imebaki miezi mitano. Sipendi kuzungumzia timu nyingine kwa kuwa mimi ni mtu ninayefuata weledi,” alisema Logarusic bila kukataa au kukubali kama amefanya mazungumzo na Yanga.
Imeelezwa viongozi wa Yanga wamefurahishwa na kazi yake siku Simba ilipoilamba Yanga kwa mabao 3-1 katika mechi ya Nani Mtani Jembe, huku akionyesha hajali nani ni staa kwenye timu na aliyeharibu, mara moja alisukumizwa kwenye benchi.

1 COMMENTS:

  1. kwani hao yanga kwann wanapenda sana kuwachimba simba kwann wasitafute kocha wao wenyewe kwann wangoje simba wawaletee ndo wachukue au wanamatatizo ya akili?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic