Nguvu ya nyota ya kipa Juma Kaseja
imeendelea kung’ara katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa
Bora Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Katika mazoezi yaliyofanyika juzi na
jana, rundo la mashabiki ‘kijiji’, liliacha kuangalia mazoezi ya wachezaji wa
ndani na kuhamia alipokuwa Kaseja.
Mashabiki hao walionyesha wamepania
kumuona kwa karibu, hivyo idadi kubwa walihamia upande aliokuwa akijifua pamoja
na kipa Ally Mustapha ‘Barthez’, wote wakiwa chini ya kocha wao, Razak Siwa,
raia wa Kenya.
Awali, mashabiki hao walikuwa upande
mmoja wakishuhudia mazoezi ya Yanga kwa ujumla, lakini walipoona mazoezi ya
makipa yameanza, wote walihamia huko huku kila mmoja akisisitiza alitaka
kumuona Kaseja akijifua.
Pamoja na nyota yake kung’ara zaidi,
Kaseja alionekana kuchoka sana na baadaye Siwa alisema ilitokana na kutofanya
mazoezi kwa kipindi kirefu.
“Amejitahidi sana, wengine huishia
katikati,” alisema Siwa.
Baada ya hapo, timu zilipangwa na Kaseja
na Barthez, kila mtu akachukua milingoti miwili.
Hadi mwisho wa mazoezi, Kaseja alifungwa
bao moja huku Barthez akifungwa mawili na timu yake kulala kwa 2-1.
Didier Kavumbagu na Simon Msuva ndiyo
walimtungua Barthez na mkongwe Nizar Khalfan akamtungua Kaseja.
0 COMMENTS:
Post a Comment