Kocha wa Makipa wa Simba,
James Kisaka, yuko hoi kitandani, lakini amewaomba viongozi wa timu hiyo kumsaidia
ili aiokoe afya yake.
Akizungumza nyumbani
kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam, Kisaka alisema hadi hivi sasa ameshatibiwa
katika hospitali kubwa tatu za Muhimbili, CCBRT na Mwananyamala, Dar bila
mafanikio ya kupona.
Kisaka alisema kwa sasa hawezi kutembea mwenyewe
kutokana na hali yake mbaya kiasi cha kusababisha kuishiwa nguvu upande wa
kushoto wa mwili wake ambapo hivi sasa anasaidiwa kutembea na mwanaye
Christopher mwenye umri wa miaka saba pamoja na mkewe, Upendo.
“Hali yangu kama unavyoiona hapa siwezi
kutembea mwenyewe, huu upande mmoja nikijaribu kutembea ni kama natetemeka hivi,
nikijaribu kutembea kwa kujilazimisha ninaweza kuanguka, msaada mkubwa kwangu ni
mwanangu huyu unayemuona na mke wangu.
“Sitaki kuonyesha naombaomba lakini
nahitaji msaada wa viongozi wa timu yangu (Simba) na yeyote atakayeguswa na
hili, nadhani sasa wakati huu ndiyo unaweza kujua wangapi walikuwa
wanakuthamini, sichagui wa kunisaidia, yeyote atakayeguswa naomba anikimbilie,”
alisema Kisaka.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment